Sinema Ya YESU
Yamkini umeona sinema nyingi lakini
sinema ya Yesu ni ya tofauti. Ni wasilisho la moja kwa moja la maisha ya
YESU na kikawaida linabadilisha maisha.
YESU ni sinema ilitotafsiriwa kwa lugha nyingi kuliko sinema ingine katika historia. Sababu yake ya
kufuzu ulimwenguni kote na
kuvutia watu ni ukweli yake; jinsi inavyo ambatana na vile kulivyotendeka na
jinsi ilivyoiga kila kitu kwa makini sana.
Injili kama alivyoandika Luka katika Biblia Takatifu ilichaguliwa kama
asili ya mazungumzo na pia uigaji kwenye sinema hii. Miaka mitano ya utafiti
ya makini na matayarisho yalifanywa kabla picha za sinema hii
hazijachukuliwa huko nchini mwa Israeli. Wanatafiti mbalimbali, wanahistoria
na wanatheologia walishauriwa. Mitambo maalumu ilitengeneza vyungu,
vifaa na nguo kama zile zilizotumika Karne ya kwanza.
"Kuchagua waigizaji kuiga maisha ya wakati wa Yesu ilifanywa kwa makini
sana, haswa yule aliyechaguliwa kuiga Yesu. Kupata nyuso zilizofaa,
waigizaji 45 walioonyeshwa sana kuliko wengine, na wengine zaidi ya
5,000 wote walichaguliwa kutoka watu walioishi sehemu ya ulimwengu ya
Mashariki ya Kati. Brian Deacon, kutoka kampuni ya Royal Shakespeare huko
Uingereza, ndiye aliyechaguliwa kuigiza Yesu. Deacon alichaguliwa kutoka
kikundi cha watu 1000 kwa sababu ya jinsi alivyoigiza vizuri hadithi ya Yesu
kama
vile ilivyoandikwa katika Injili na Luka Mtakatifu."
Hadi wa leo, sinema ya YESU imetafsiriwa hadi lugha zaidi ya
723. Watu zaidi ya bilioni 4 wameiona kote ulimwenguni. Sinema hii ilidhaminiwa na Campus Crusade for Christ
International. Upigaji wa picha uliongozwa na John Heymann, mshindi wa
zawadi katika Cannes Film Festival. Kampuni ya Warner Brothers ndiyo
iliyosimamia kutolewa kwa picha hii kwa mara ya kwanza huko Kaskazini ya Marikani.
|