Tembea sehemu yoyote ulimwenguni. Ongea na watu wa
dini yoyote. Haijalishi jinsi walivyoshikilia tabaka za dini zao, kama
wanajua chochote kuhusu historia, watakubali kwamba hakujawahi kuwa na mtu
kama Yesu wa Nazareti. Yeye ni mtu wa ajabu mno kuliko watu wote wa enzi
zote.
Yesu alibadilisha mwenendo wa historia. Hata tarehe kwenye gazeti lako la
leo inathibitisha kwamba Yesu wa Nazareti aliishi ulimwenguni karibu miaka
2,000 iliyopita. Maandishi kwa Kiingereza "B.C." yanasimamia nyakati kabla
ya kuzaliwa kwa Kristo; vilevile maandishi "A.D." yanasimamia nyakati baada
ya kuzaliwa kwa Kristo.KUJA KWAKE KULITABIRIWA
Mamia ya miaka hata kabla ya Yesu kuzaliwa, maandiko yaonyesha wanabii wa
Israeli wakitabiri kuja kwake. Agano la kale, lililoandikwa na watu wengi
katika muda wa miaka 1,500, lina unabii zaidi ya 300 kuhusu kuja kwa Yesu.
Yote yaliyotabiriwa yalitendeka, pamoja na kuzaliwa kwake kimiujiza, maisha
yake matakatifu, kufa na kufufuka kwake.
Maisha aliyoishi Yesu, miujiza aliyotenda, maneno aliyosema, kufa kwake
msalabani, kufufuka kwake, kupaa kwake mbinguni - yote yathibitisha kwamba
yeye hakuwa mwanadamu peke yake bali alikuwa zaidi ya mwanadamu. Yesu
alisema, "Mimi na Baba tu umoja" (Yohana 10:30), "Aliyeniona mimi
amemwona Baba" (Yohana 14:9) na, "Mimi ndimi njia, na ukweli, na uzima;
mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi." (Yohana 14:6).
MAISHA NA UJUMBE WAKE HUSABABISHA MABADILIKO

Tazama maisha na mvuto wa Yesu wa Nazareti, Mesiya, katika historia yote
na utaona kwamba yeye na ujumbe wake huleta mabadiliko makubwa katika
mataifa na maisha ya wanaume na wanawake. Popote mafunzo yake yalipoenea,
utakatifu wa ndoa, haki na sauti ya wanawake imetiliwa maanani; shule na
vyuo vikuu vimeanzishwa; sheria za kulinda watoto zimeandikwa; utumwa
umeachishwa; na mabadiliko mengine mengi yamefanywa kwa manufaa ya wanadamu.
Maisha ya watu binafsi yamebadilishwa kiajabu. Kwa mfano, Lew Wallace,
jemedari aliyejulikana na mwandishi shupavu, alikana Mungu yupo. Kwa miaka
miwili, Bw. Wallace alisoma kwenye maktaba zilizo bora sana kule Ulaya na
Merikani, akitafuta habari ambazo zingeangamiza kabisa dini ya Kikristo.
Alipokuwa akiandika sura ya pili ya kitabu hicho, alijikuta ghafla
ameanguka magotini na kulia kwa Yesu akisema, "Bwana na Mungu wangu."
Kwa sababu ya ushuhuda usioweza kukanwa, hakuweza kuendelea kukana kwamba
Yesu Kristo alikuwa mwana wa Mungu. Baadaye, Lew Wallace aliandika kitabu
kilichoitwa "Ben Hur", moja wapo ya vitabu shwari vilivyo andikwa katika
lugha ya Kiingereza kuhusu nyakati za Kristo.
Vile vile, marehemu C. S. Lewis, profesa wa chuo kikuu cha Oxford,
alikana kwamba Kristo alikuwa pia Mungu kwa miaka mingi. Lakini, yeye pia,
kwa hekima za ukarimu, alijinyenyekeza mbele za Yesu kama Mungu na Mwokozi
baada ya kusoma ushahidi usio na pingamizi kwamba Yesu pia alikuwa Mungu .
BWANA, MWONGO AU MWENDA WAZIMU?
Katika kitabu chake kilichojulikana sana "Mere Christianity", Lewis
aliandika, "Mtu ambaye alikuwa mwanadamu peke yake na kusema maneno kama
aliyoyasema Yesu hawezi kamwe kuwa mwalimu wa utu wema. Huenda ikawa alikuwa
mwenda wazimu - sawasawa na mtu anayesema kwamba yeye ni yai lililochemshwa -
au roho chafu kutoka kuzimu. Wewe lazima uchague. Kama yeye alikuwa, na hata
sasa ni Mwana wa Mungu, au yeye ni mwenda wazimu au kitu kibaya zaidi.
Unaweza kumwita mpumbavu au unaweza kujinyenyekeza chini ya miguu yake na
kumwita Bwana na Mungu. Lakini tusije na maneno hohehahe tukisema kwamba
yeye alikuwa mwalimu shupavu wakibinadamu tu. Yeye hajaacha hilo chaguo wazi
kwetu."
Yesu wa Nazareti ni nani kwako? Maisha yako ya hapa duniani na pia ya uzima
wa milele yatategemea jibu lako kwa swali hili.
Dini zote zingine zilianzishwa na wanadamu na zinategemea falsafa za kibinadamu, kanuni na pendekezo za tabia. Ondoa waanzilishi wa dini hizi
kutoka idhini na tabaka za kuabudu, na machache sana yatabadilika. Lakini
ondoa Yesu Kristo kutoka Ukristo na hakuna chochote kitakachobaki. Ukristo
uliopendekezwa kwenye Biblia siyo falsafa ya maisha peke yake, wala siyo
tabaka na njia za kimila za kuabudu. Msingi wa Ukristo wa kweli ni
uhusiano wa kibinafsi na Mwokozi na Bwana aliyefufuka na anayeishi.
MWANZILISHI ALIYEFUFUKA
Yesu wa Nazareti alisulubiwa, akazikwa kwenye kaburi lililokopwa, na siku
ya tatu alifufuka kutoka wafu; Ukristo niwa kipekee kwa ajili ya jambo hili.
Ubishi wowote juu ya ukweli wa Ukristo utategemea uthibitisho wa kufufuka kwa
Yesu wa Nazareti.
Katika enzi zote, waliohitimu katika masomo na kuchunguza sana mathibitisho ya
ufufuo wameamini, na wangali wanaamini kuwa Yesu yuhai. Baada ya kuchunguza
mathibitisho ya ufufuo kama yalivyoandikwa na waandishi wa Injili, marehemu
Simon Greeleaf, aliyehitimu kwa mambo ya kisheria katika Harvard Law School,
alisema; "Haingewezekana kamwe kwao kuendelea kusisitiza ukweli wa mambo
walionena, kama Yesu kweli hakufufuka kutoka wafu, na kama hawakujua jambo
hili kama walivyojua ukweli wowote mwingine walioujua kwa uhakika.
John Singleton Copley ambaye ni mwanasheria aliyetambulikana sana,
alisema: "Najua kiasi kwamba ushahidi ni kitu gani; nakwambia, ushahidi kama
ule uliotolewa kuthibitisha ufufuo bado haujawahi kuvunjwa."
SABABU ZA KUAMINI
Ufufuo ni msingi katika imani ya Mkristo. Kuna sababu kadha wa kadha ambazo
wale wanaosoma kuhusu ufufuo wanaamini kuwa ufufuo ulitendeka:
KUTABIRIWA:
Kwanza, Yesu alitabiri habari za kifo chake na ufufuo na zikatendeka kadri na jinsi
alivyotabiri ( Luka
18:31-33).
KABURI LILIYO WAZI: La pili, ufufuo ni kielelezo cha pekee
cha
kaburi lililo wazi. Ukisoma Biblia kwa makini, utaona kwamba kaburi ambalo
walilolaza mwili wa Yesu lililindwa barabara na wanajeshi wa Kirumi na pia
lilizibwa na jiwe. Kama Yesu hakuwa amekufa, bali alikuwa amedhoofika - kama
wengine walivyosema, walinzi na jiwe pia lingezuia juhudi za kuhepa au kusaidiwa
na wafuasi wake. Maadui wa Yesu hawangechukua mwili kwa sababu kukosekana
kwa mwili huo pale kaburini ingalitia nguvu imani juu ya kufufuka kwake.
KUONANA KIBINAFSI: La tatu, ufufuo ni kielelezo cha
kipekee cha kuonekana kwa Yesu na wafuasi wake. Baada ya kufufuka kwake,
Yesu alionekana mara zisizopungua 10 na wale waliomjua na pia kwa watu
500 waliokusanyika pamoja. Bwana aliwathibitishia kwamba kuonekana kwake mara tatu
hizikuwa ndoto. Alikula na kuongea nao na walimgusa (
1 Yohana 1 :1).
KUZALIWA KWA KANISA: La nne, ufufuo ni sababu ya pekee ya
kueleza sababu ya kanisa kuanzwa. Kanisa la Kristo ni chama kikubwa kuliko
vingine vilivyoko sasa pia vilivyowahi kuwepo katika historia ya ulimwengu.
Zaidi ya nusu ya mahubiri ya kwanza yaliyohubiriwa yalikuwa kuhusu ufufuo (Matendo
2:14-36). Hakika kanisa la kwanza lilijua kwamba jambo hili litakuwa
msingi wa ujumbe wake. Maadui wa Yesu wangelikomesha wakati wowote kwa kuutoa
mwili wa Kristo.
MAISHA YALIYOBADILISHWA: La tano, ufufuo ni kielelezo cha kipekee
cha maisha yaliyobadilishwa ya wafuasi wake. Walimwacha kabla ya kufufuka
kwake; baada ya kifo chake walikufa moyo na kuogopa. Hawakutarajia kwamba
Yesu atafufuka kutoka wafu (Luka
24 :1-11).
Lakini baada ya kufufuka kwake na mambo waliyopata wakati wa Pentekote, hawa
waliokufa moyo, waliopoteza hamu, wanaume kwa wanawake, walibadilishwa na
nguvu za Kristo aliyefufuka. Katika jina lake, walifanya kishindo kikubwa
duniani. Wengi walipoteza maisha yao kwa ajili ya imani yao; wengine
waliudhiwa vibaya. Matendo yao ya ujasiri hayana kielelezo kamili isipokuwa
kwamba waliamini Yesu Kristo kweli alifufuka kutoka wafu - jambo
lililowatosha hata kukubali kufa kwa ajili yake.
Katika miaka 40 ya kufanya kazi na wataalamu wa vyuo vikuu ulimwenguni,
sijawahi kukutana na mmoja ambaye ameyasoma mathibitisho ya dhati kuonyesha
uungu wa Yesu wa Nazareti na pia kufufuka kwake, ambaye hakukubali kwamba yeye ni
Mwana wa Mungu, Mesiya aliyeahidiwa. Ijapokuwa wachache hawaamini, wanasema
kwa moyo wa kweli, "Sijachukua muda wowote kusoma Biblia au kuangalia mambo
katika
kihistoria yalitotendeka katika maisha ya Kristo."
BWANA
ANAYEISHI: Kwa sababu ya ufufuo wa Yesu, wanafuasi wake wa
kweli hawafuati tu orodha za mwanzilishi aliyekufa, bali wanauhusiano wa
karibu na wakibinafsi na bwana aliyehai. Yesu Kristo yuhai leo na anabariki na
kuimarisha maisha ya wote wanaomwamini na kumtii. Katika enzi zote, wengi
wamedhihirisha kufa kwake Yesu Kristo, kati yao wakiwa watu waliotenda
makuu ulimwenguni.
Mwanafizikia na mwanafalsafa wa Kifaransa Blaise Pascal alisema jinsi mwanadamu anavyomhitaji Yesu aliposema, "Kuna pengo katika moyo wa kila
mwanadamu linayoweza kuzibwa na Mungu peke yake kupitia Mwana wake Yesu
Kristo."
Je, ungependa kumjua Yesu Kristo kama Mwokozi
wako? Unaweza! Yesu anahamu ya kuanza uhusiano wa kibinafsi uliojaa upendo
kwako. Ameshafanya matayarisho yote.
Kujua jinsi ya kuanza uhusiano na Kristo aliyehai,
bonyeza hapa... |